Uingereza
ALIYEKUWA Gavana wa mojawapo wa majimbo yanayozalisha mafuta kwa wingi nchini Nigeria , James Ibori, amekiri katika mahakama ya Uingereza mashtaka kumi ya kuhusika na biashara haramu ya fedha na pia njama ya kughushi.
Polisi wa Uingereza wanamshtumu Ibori kwa kuiba takriban dola milioni 400 katika kipindi cha miaka 8. Ibori, ambaye wakati mmoja alichukuliwa kuwa mmojawapo wa wanasiasa tajiri na mwenye ushawishi mkubwa alikamatwa mnamo mwaka 2007.
Baadaye aliachiliwa kabla ya kukamatwa tena mjini Dubai kutokana na hati ya Uingereza na kusafirishwa hadi nchini humo. Mnamo mwaka 2007, mahakama ya Uingereza ilipiga tanji mali zake zote zilizoshukiwa kuwa za thamani ya dola milioni 35. Mshahara wake kama gavana wa jimbo la Delta ulikuwa chini ya dola 25,000.
Historia yake
James Onanefe Ibori amezaliwa 4 Agosti 1958, alikuwa Gavana wa Jimbo la Delta nchini Nigeria kutoka Mei 29, mwaka 1999 hadi Mei 29, 2007. Ni mwanachama wa chama tawala cha People’s Democratic Party (PDP). Alikuwa msemaji zaidi katika mijadala ya kitaifa ya rasilimali nchini Nigeria .
Maisha ya awali
Alizaliwa katika familia ya marehemu Chief Ukavbe Ibori na Bi Faraja Oji Ibori wa Otefe katika ukoo wa Oghara, Halmashauri ya Ethiope Magharibiya Jimbo la Delta. Alisoma katika shule ya sekondari ya Baptist, Oghareki, kwa sasa inaitwa Oghareki Grammar School , kabla hajaendelea katika Chuo Kikuu cha Benin ambapo alipata Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya uchumi na takwimu. Alianza kazi yake katika kampuni ya Mobil Oil Nigeria Limited na baadaye katika Shirika la Taifa la Mafuta la Nigeria (NNPC) kama mmoja wa wafanyakazi waanzilishi.
Kati ya mwaka 1994 na 1997, alikuwa mshauri wa Serikali ya Shirikisho katika maeneo ya uundaji sera ya umma na utekelezaji wake. Jukumu lake kubwa katika kipindi hiki lilikuwa utafiti, ambao ulisababisha uundaji wa sera ya taifa ya dawa za kulevya katika nchi.
Kazi ya siasa
Kazi ya siasa kwa Ibori ilianza mwaka 1990 alipojiunga na National Republican Convention (NRC). Mwaka 1991, aliteuliwa kugombea nafasi ya uwakilishi, akiwakilisha Jimbo la Ethiope. Alipoteza nafasi hiyo iliyokwenda kwa mgombea wa Social Democratic Party (SDP). Mpango wa Mpito wa Sani Abacha ulipotupwa, alijiunga na Grassroots Democratic Movement (GDM). GDM kilikuwa na idadi ya nafasi katika serikali za mitaa, majimbo na serikali ya shirikisho, ikiwa ni pamoja na moja ya viti vitatu vya useneta katika jimbo. Programu ya mpito ilisitishwa ghafla kutokana na kifo cha Abacha. Baadaye Ibori na viongozi wa makundi mengine ya kisiasa katika Jimbo la Delta, walianzisha chama cha Delta National Congress (DNC).
DNC baadaye kiliungana na vingine vyenye mtazamo na mawazo kama yao na kuzaliwa Peoples Democratic Party (PDP). Ilikuwa ni kwenye jukwaa la PDP ambapo aligombea na kushinda katika uchaguzi wa Januari 9, 1999 na kuwa gavana wa Jimbo la Delta. Mwaka 2003, alichaguliwa tena kuwa gavana kwa muhula mwingine wa miaka minne.
Mashtaka ya ufisadi
Uingereza
Kutokana na madai ya rushwa, mahakama nchini Uingereza ilizuia mali yake huko, yenye thamani ya zaidi ya pauni milioni 17 (dola milioni 35), mwanzoni mwa Agosti 2007.
Mke wake, Nkoyo, alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow mjini London tarehe 1 Novemba 2007, ili kuchunguza mali ya mume wake, hasa nchini Uingereza. Aliachiwa baada ya maswali.
Katika mahojiano maalum na CNN, Ibori alikanusha madai dhidi yake akidai yalikuwa kisiasa. Alimshutumu Ribadu (Nuhu Ribadu) na Mahakama ya Uingereza kwa siasa.
These corruption charges brought against Ibori by the government of former President Obasanjo are among many begun by anticorruption czar Nuhu Ribadu against former officials of the ruling Peoples Democratic Party PDP. Ribadu additionally alleged that Ibori attempted to bribe him to drop the charges with a cash gift of $15 million, which he (Ribadu) immediately lodged in the Central Bank of Nigeria CBN. The cash remains in the CBN as an exhibit. Desemba 12, 2007, Ibori alikamatwa na Tume ya Uhalifu wa Fedha na Uchumi (EFCC) katika Hoteli ya Kwara State , Asokoro, katika Abuja . Mashtaka aliyokumbana nayo ni pamoja na wizi wa fedha za umma, matumizi mabaya ya ofisi, na kujihusisha na masuala ya fedha. Madai haya ya rushwa yaliyoletwa dhidi ya Ibori na serikali ya Rais wa zamani, Obasanjo ni miongoni mwa mengi yaliyoanzishwa na Nuhu Ribadu dhidi ya maofisa wa zamani wa chama tawala cha Peoples Democratic Party (PDP). Ribadu aliongeza madai kuwa Ibori alijaribu kumhonga ili aachane na mashtaka pamoja na zawadi ya fedha taslimu ya dola milioni 15, ambayo yeye (Ribadu) aliipeleka Benki Kuu ya Nigeria (CBN) mara moja. Fedha ilibakia CBN kama ushahidi.
kuachiwa
Desemba 17, 2009, Mahakama Kuu ya Shirikisho iliketi mjini Asaba, Jimbo la Delta, na kumuachia huru Ibori katika mashtaka yote 170 ya rushwa yaliyoletwa dhidi yake na EFCC.
EFCC ilifungua taarifa ya rufaa dhidi ya hukumu ya Desemba 17, 2009 na imeanza duru mpya ya uchunguzi juu ya gavana wa zamani kufuatia malalamiko kutoka kwa wazee wa Jimbo la Delta, Viongozi na Wadau wa Jukwaa, ambayo yalitolewa na umma mnamo Machi 2010.
Mashtaka mapya
Aprili 2010, miezi mitatu baada ya serikali na Goodluck Jonathan kuchukua nafasi, faili la kesi ya Ibori lilifunguliwa tena. Madai mapya ya wizi wa Naira bilioni 40 (dola milioni 266) yalifunguliwa dhidi yake. Majaribio ya kumkamata hayakufanikiwa. Iliripotiwa kuwa alikimbia kutoka Abuja hadi Lagos na kisha Oghara, katika eneo la kwao la Niger Delta. Iliripotiwa kuwa amekuwa akilindwa na wanamgambo wenye silaha na waliwahi kupambana kwa risasi na vikosi vya usalama vya serikali. Alidai kuwa madai yalikuwa ya kijinga na kwamba alikuwa mwathirika wa mateso ya kisiasa.
Aprili 25, 2010, kulikuwa na taarifa kwamba Ibori aliikimbia nchi kukwepa kukamatwa na ushirika wa EFCC. Mkuu wa Vyombo vya Habari na Uenezi wa EFCC, Femi Babafemi, alithibitisha kuwa tume ilikuwa ina ripoti ya kiusalama ambapo Ibori aliikimbia Nigeria , na aliongeza kuwa msaada wa Interpol utahitajika ili kusaidia kukamatwa kwake. 30 Aprili, 2010, ripoti ya usalama ilionesha kuwa madai ya kutoroka Ibori kutoka Nigeria yanaweza kuwa geresha. Mashirika ya Usalama yalihisi alikuwa bado katika maficho nchini Nigeria . Gazeti la Compass lilitoa habari Julai 12, 2010 kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria (CBN), Malam Sanusi Lamido amebaini kuwa James Onanefe Ibori alitumika Jimbo la Delta kama dhamana kwa ajili ya mkopo wa Naira bilioni 40 alipokuwa gavana wa Jimbo.
Kutiwa mbaroni na INTERPOL mjini Dubai
Habari za ukurasa wa mbele wa gazeti la Punch la Mei 13, 2010 zilisema kuwa "dalili zilijitokeza siku ya Alhamisi kwamba Chief Ibori James anaweza kuwa amekamatwa mjini Dubai, U.A.E na mawakala wa INTERPOL kwa kuzingatia hati ya kukamatwa ya kimataifa iliyotolewa na serikali ya Uingereza kwa mujibu wa madai ya kujihusisha na fedha haramu".
Tarehe 1 na 2 Juni 2010, mahakama ya Uingereza ilimuona dada wa James Ibori, Christine Ibie-Ibori, na mshirika wake, Udoamaka Okoronkwo, kuwa na hatia ya makosa ya kujihusisha na fedha haramu katika hukumu iliyotolewa katika Mahakama ya Southwark Crown, London . James Ibori, kupitia msaidizi wake alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akihoji uhalali na kupinga maamuzi ambayo alidai kuachiwa hurfu kwa wanawake wengine wawili, Bi Okoronkwo na Adebimpe Pogoson ambao walishtakiwa pamoja na dada yake. Uamuzi wa mahakama wa Juni 2, 2010 hata hivyo ikarudia uamuzi dhidi Okoronkwo. Chrstine Ibie-Ibori na Udoamaka Okoronkwo walifungwa kifungo cha miaka 5 jela kila mmoja, Jumatatu Juni 7, 2010 na mahakama ya Uingereza hata kama wakili alisihi waonewe huruma kwamba walidanganywa na James Bori.
James Ibori alikabidhiwa kwa mamlaka ya Uingereza mjini Dubai na kusafirishwa hadi Uingereza Aprili 15, 2011. Mnamo Februari 2012 alikiri kuwa na hatia ya makosa 10 ya kujihusisha na fedha na njama za udanganyifu. Atahukumiwa Aprili, 2012.
Makala haya yameandaliwa na Bishop Hiluka kwa msaada wa vyanzo mbalimbali vya habari vya kimataifa.
No comments:
Post a Comment