Bosco Ntaganda
DRC
VIKOSI vinavyomtii muasi wa
jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , Bosco Ntaganda, anayetafutwa na Mahakama ya
Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) vimeteka miji miwili ya mashariki mwa DRC.
Mwandishi wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC) katika eneo hilo alitoa taarifa kuwa maelfu ya watu walikimbia mapigano
makali na kuelekea karibu na mjini Goma.
Mamia ya askari wenye
silaha nzito wanaomtii Jenerali Ntaganda hivi karibuni walijitenga kutoka jeshi
la nchi hiyo. Akiwa anafahamika kama ‘Terminator,’
Jenerali Ntaganda amekanusha tuhuma za ICC kuwa aliwasajili watoto kuwa askari.
Mwandishi wa BBC, Thomas
Hubert, akiwa eneo la Sake, kilometa 30 (18 maili) magharibi mwa Goma, alisema kuwa
wakazi wamemwambia wamesikia mapigano kati ya vikosi vya Jenerali Ntaganda na
vikosi vya serikali yakiendelea Jumapili iliyopita usiku.
Askari wa serikali
walirudishwa nyuma na kuondolewa katika miji ya Mushake na Karuba, na wamerudi
nyuma kwa kilometa 12 mashariki mwa mji wa Sake, ambako walianza kujikusanya
kupambana naye.
Askari hao waasi walikimbia
jeshi la Congo lenye ngome yake Goma mapema mwezi huu, idadi kati
ya 400-500, kwa mujibu wa vyanzo vya UN na Majeshi ya DRC.
Katika mapigano mengine
katika eneo la kaskazini la Kivu ya Kaskazini kati ya majimbo ya Mweso na
Kitchanga, maafisa wa jeshi la Congo walisema kuwa wamesimamisha shughuli za watu wa
Jenerali Ntaganda.
Kati ya mwaka 2002-2005,
Jenerali Ntaganda alikuwa mkuu wa harakai za kijeshi wa waasi wa UCP
wakiongozwa na mbabe wa kivita, Thomas Lubanga – ambaye mwezi Machi alikuwa wa
kwanza kukutwa na hatia na mahakama ya ICC baada ya kukutwa na hatia ya
kusajili watoto kuwa aksari.
Jenerali Ntaganda mtuhumiwa
mwenza – lakini Rais Joseph Kabila awali alikataa kukamatwa kwake kwa ajili ya
amani ya DRC. Hata hivyo, Rais kabila mapema mwezi huu alitoa wito wa kukamatwa
kwake ingawa anasema hatampeleka ICC.
Licha ya kumalizika kwa
vita vya DRC mwaka 2003, makundi kadhaa yenye silaha bado yanazunguka katika
eneo lenye utajiri mkubwa wa madini mashariki mwa nchi licha ya UN na jeshi la
nchi hiyo kuwanyang’anya silaha.
Huku hayo yakiendelea,
kiongozi wa mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Luis Moreno
Ocampo, ametoa ombi la kukamatwa kwa kiongozi wa kundi la wanamgambo wa kihutu
la FDLR katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo , Sylvestre Mudachumura na pia anataka mashtaka
mapya kufunguliwa dhidi ya Jenerali Bosco Ntaganda.
Ocampo anasema kuwa
Sylvestre Mudacumura, ni kiongozi wa waasi ambaye kwa sasa anahangaisha raia
katika eneo la Mashariki mwa Congo . Wote wawili sasa wanasakwa ili kujibu mashitaka
uhalifu dhidi ya binadamu , uhalifu wa kivita, mauaji na ubakaji.
Hiostoria yake
Bosco Ntaganda alizaliwa
1973 nchini Rwanda . Ni kiongozi wa vikosi vilivyofanya mauaji ya Kiwanji mwaka 2008, na
mkuu wa jeshi la Mkusanyiko wa Kitaifa kwa ajili ya Ulinzi ya Watu (CNDP), kikundi
cha wanamgambo wanaoendesha vita katika Kivu ya Kaskazini katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC). Ni mwanachama wa zamani wa Rwanda Patriotic Army na anadaiwa kuwa alikuwa Naibu Mkuu
wa Watumishi wa Majeshi ya Ukombozi wa Congo (FPLC).
Mei 2008, alikuwa anatafutwa
na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya uhalifu wa kivita kwa kuhusisha
na kuwasajiri watoto chini ya umri wa miaka kumi na tano na kuwatumia kushiriki
kikamilifu katika mapambano.
Pia anajulikana kama "Terminator" na jina lake wakati mwingine hutolewa kama Tanganda, Ntanganda, Ntangana, Ntagenda, Wabaganda au Taganda. Ntaganda
alipigana akiwa na Rwanda Patriotic Army mwanzoni mwa miaka ya 1990 na
kushiriki katika kuangushwa kwa serikali iliyoongozwa na Wahutu wa Rwanda mwaka 1994.
Hatimaye alijiunga na Majeshi
ya Ukombozi wa Congo (Forces Patriotiques pour la Liberation du Congo, FPLC), na kuwa mkuu
wake wa shughuli za kijeshi. Wakati huo, amedaiwa kuhusika katika mauaji
mbalimbali na mengine ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Januari 2005, Ntaganda
aliteuliwa kuwa generali katika Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kama sehemu ya mchakato wa amani, lakini alikataa nafasi
hiyo. Tarehe 1 Novemba 2005, kamati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
ilipiga marufuku kusafiri na kuzuia mali kwa sababu ya kukiuka vikwazo vya silaha.
Mwaka 2006, kufuatia
migogoro ndani ya UPC, alirudi Kivu Kaskazini, mkoa wake wa nyumbani, na
kujiunga na Laurent Nkunda katika National Congress for the Defense of the
People (CNDP). Aprili 2008, aliaminika kuishi wilaya ya Masisi ya Kivu
Kaskazini, akihudumu kama mkuu wa wafanyakazi wa CNDP. CNDP sasa imekuwa
ikifanya kazi mara kwa mara Kongo na Ntaganda sasa ni kama Mkuu wa jeshi, pamoja na kutakiwa na ICC.
Mwaka 2012, anaishi kwa uwazi
katika mji wa Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, katika eneo la Avenue
des Tulipiés, kama yadi 100 kutoka mpaka wa Rwanda .
Kwa mujibu wa mamlaka ya DRC,
Jenerali Bosco Ntaganda "alivuka kutoka Goma hadi katika mji wa Gisenyi , Rwanda , mara mbili katika mwaka 2011, mwezi Machi na
Septemba, pamoja na kuwepo marufuku ya kusafiri yaliyopigwa juu yake. Mamlaka
ya Kongo ilitoa taarifa kwamba mara zote mbili Ntaganda alikuwa amekwenda huko
kuhudhuria mazishi, baada ya kuigundua idhini rasmi ya kufanya hivyo kutoka kwa
uongozi wake wa kijeshi na kutoka mamlaka uhamiaji. Maafisa wa Rwanda walisema kwamba hawakuwa na pingamizi kwa Ntaganda
kuvuka mpaka. Wanadai kwamba hali yake kama mtu binafsi "si tatizo la Rwanda , lakini ni tatizo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ", na kuongeza kwamba "Bosco huchangia
amani na usalama katika mkoa, ambayo inaendana na malengo ya Rwanda ".
Kundi la Wataalamu wa Umoja
wa Mataifa lilitoa taarifa mwishoni mwa mwaka 2011 kwamba Ntaganda anadhibiti eneo
la Mungwe na migodi ya Fungamwaka, karibu na Numbi, kupitia Kampuni ya Madini
ya Great Lakes , na kusimamiwa na Edson Musabarura. Ntaganda pia anapata
faida kutokana na uchimbaji wa madini katika eneo la Nyabibwe, kwa njia ya
muungano wake pamoja na Kanali Saddam Ringo. Katika eneo la Rubaya, Ntaganda anapata
mapato makubwa kutokana na kodi inayotozwa na polisi wa madini walio "sambamba".
Ntaganda aliamuru askari wake kuingilia kati kwa niaba ya Congo Krall Metal
katika eneo la Lueshe.
Aprili 4, 2012, iliripotiwa
kwamba Ntaganda na askari mwaminifu 300 walijiondoa kutoka DRC na walipambana
na majeshi ya serikali katika eneo la Rutshuru kanda ya Kaskazini ya Goma. Aprili
11, 2012 Rais Kabila alitoa wito wa kukamatwa Ntaganda.
Tarehe 22 Agosti 2006,
Mahakama ya utangulizi ya ICC ilibaini kuwa kuna busara ya kuamini kwamba
Ntaganda anahusika katika jinai kwa uhalifu wa kivita uliofanywa na FPLC kati
ya Julai, 2002 na Desemba 2003, na ilitoa kibali cha kukamatwa kwake.
Alishtakiwa kwa uhalifu wa kivita kuhusisha na kuwasajiri watoto chini ya umri
wa miaka kumi na tano na kuwatumia kushiriki kikamilifu katika mapambano.
Waasi wengine watatu wa
Kongo, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa UPC, Thomas Lubanga, wapo chini ya ulinzi
wa ICC.
Makala haya yameandaliwa na Bishop Hiluka kwa msaada
wa vyanzo mbalimbali vya habari vya kimataifa.
No comments:
Post a Comment