Mary Keitany
Wilson Kipsang
Uingereza
WILSON Kipsang na Mary
Keitany kutoka Kenya walichukua ushindi kwa kishindo katika mashindano ya Jumapili ya iliyopita
katika mbio za London Marathon mwaka 2012. Katika mbio za wanaume, Kipsang
aliweza kuongoza katika maili saba za mwisho, na ilikuwa nusra avunje rekodi ya
mashindano ya London .
Alimaliza kwa muda usiokuwa
rasmi wa saa 2:04.44. Mkenya mwenzake Martin Lel alifanikiwa kumpita
mwanariadha wa Ethiopia , Tsegaye Kebede, na ambaye ameshawahi kuwa mshindi
wa mashindano ya London , na kumaliza katika nafasi ya pili, ikiwa ni kasi
ya juu mno katika kumalizia mashindano.
Kebede, aliyemaliza wa
tatu, alifanikiwa kuwazuia Wakenya kuzoa nafasi zote tatu za mwanzo kwa upande
wa mbio za wanaume, lakini kwa upande wa kina dada juhudi za Waethiopia
hazikufanikiwa kwani mkenya mwingine, Mary Keitany alifanikiwa kuhifadhi
ubingwa wake kwa mwaka wa pili mfululizo, kwa kushinda katika muda wa 2:18.37.
Historia ya Wilson Kipsang Kiprotich
Wilson Kipsang Kiprotich amezaliwa tarehe 15 Machi 1982. Ni mkimbiaji wa
mbio ndefu, anayetoa ushindani katika mbio za kuanzia km 10 hadi marathon
kamili.
Anashikilia nafasi sita kwa kasi zaidi katika mbio za nusu marathon (dakika
58:59). Nafasi yake bora katika marathoni
ni saa 2:03:42 aliyoiweka mwaka 2011 katika Frankfurt Marathon iliyomfanya
kuwa wa pili kwa kasi katika muda wote nyuma ya Mkenya mwenziye, Patrick Makau
(aliyekimbia kwa 2:03:38 ). Ni
mshindi mara mbili wa mashindano ya Frankfurt (2010 na
2011) na pia alishinda katika mashindano ya Lake Biwa Marathon na London Marathon (2012).
Kipsang anatoka Wilaya ya
Keiyo nchini Kenya , alianza ushindani wa mbio katika Polisi, na kumaliza wa pili katika
kilomita 10 za Tegla Loroupe Peace. Akaanza mbio za kimataifa mwaka 2007 na
mwaka huo alichukua nafasi ya pili katika mbio za Tilburg , akiweka rekodi ya muda wa 46:27, na alishinda mbio
za Hem (kwa muda wa 27:51 akiwa wa nne kwa kasi katika mbio za km 10 mwaka
huo). Pia alichukua nafasi ya tatu katika michuano ya Jeshi la Polisi nchini Kenya , na kumaliza nyuma ya Richard Mateelong.
Katika mashindano Bora ya
Dunia ya kilomita 10, alishika nafasi ya tatu kwa muda wa 28:09, akishindwa na
Deriba Merga na Sila Kipruto.
Alirudi katika mbio za Tilburg mwaka 2008, na kumaliza tena akiwa wa pili kwa
sekunde mbili tu nyuma ya mshindi, Abiyote Guta. Kilele chake kwa mwaka huo kilikuwa
katika Nusu Marathon za Delhi .
Kipsang alimsukuma Merga, mshindi wa World Road Champion mwaka 2006, karibu kabisa na mstari wa
kumalizia lakini alimaliza wa pili nyuma yake. Pamoja na kumaliza nafasi ya
pili, Kipsang alifurahishwa na ubora wake kwa zaidi ya dakika 59:16. Pia
alikuwa wa tatu kwa kasi katika nusu marathon kwa kwa mwaka huo, Merga na Haile
Gebrselassie wakiwa mbele yake.
Kipsang alianza kwa nguvu 2009,
kwa kushinda Nusu Marathon za Egmond katika hali ya baridi. Kazi nzuri nyingine
ni pale alipotwaa nafasi ya pili katika mbio za Nusu Marathoni za Ras Al
Khaimah - muda wake ni 58:59 uliomfanya kushika nafasi ya pili na akawa wa nne
kukimbia chini ya dakika 59. Pamoja na kuwa bora mwaka 2009 katika Nusu
Marathon ya Berlin , aliishia katika nafasi ya tatu ambayo ilikuwa ni
mara ya kwanza, ambapo wakimbiaji wote wanne wa juu kumaliza chini ya saa moja.
Alishiriki katika mashindano
ya World 10k ya Bangalore Mei 2009, na kumaliza wa nne. Alimaliza wa kwanza katika
Nusu Marathoni ya Mabingwa ya IAAF mwishoni mwa mwaka huo, na kuchukua nafasi
ya nne kwa muda wa 01:00:08 .
Mwaka 2010 alishiriki mara
ya kwanza katika mbio za Marathoni za Paris mnamo Aprili 2010, na alishika nafasi ya tatu
katika muda wa saa 2:07:13 , nusu dakika nyuma ya mshindi, Tadesse Tola. Alishinda katika marathoni
za Frankfurt mwezi Oktoba katika rekodi mpya ya saa 02:04:57 , akimshinda Tadesse kwa zaidi ya dakika. Ubora wake
mpya ulimfanya kuwa wa nane kwa kasi katika muda wote. Alishinda mbio zake za
tatu za Lake Biwa Marathon mwaka 2011, akimshinda Deriba Merga katika rekodi ya
saa 2:06:13 . Alitetea taji lake katika mbio za Frankfurt , alijitokeza
ndani ya sekunde nne, kabla ya kuvuka mstari wa mwisho kwa saa 2:03:42 , na kuwa mtu wa pili kwa kasi katika marathon kwa
muda wote.
Mwaka 2012 alianza na
kumaliza katika nafasi ya tatu katika mbio za Nusu Marathoni za RAK.
Historia ya Mary Jepkosgei Keitany
Mary Jepkosgei Keitany amezaliwa
Januari 17, 1982 katika eneo la Kisok, wilaya ya Baringo. Ni mwanariadha kutoka
Kenya wa mbio ndefu. Alishinda medali ya fedha mwaka 2007
katika Mbio za Dunia za Mabingwa za IAAF na akawa bingwa wa dunia katika Nusu Marathon
miaka miwili baadaye. Alishinda mbio za London Marathon za 2011 kwa saa 2:19:19 zikimfanya kuwa wa nne kwa kasi kwa upande wa wanawake
katika muda wote.
Rekodi yake ya muda wa saa 1:05:50 katika mbio za nusu marathoni ndiyo rekodi ya dunia
kwa wanawake. Pia anashikilia rekodi ya dunia katika maili 10 kwa wanawake (dakika
50:05), kilomita 20 (62:36), na km 25 (1:19:53 ).
Alianza kushiriki mbio alipokuwa
shule ya msingi. Mwaka 2002, alijiunga na Hidden Talent Academy . Januari 2006 alikuwa katika nafasi ya 21 katika
mbio zake za kwanza (Mbio za Wanawake za Shoe4Africa, baada ya mafanikio kadhaa
katika mashindano ya kitaifa, alishiriki nje ya nchi kwa mara ya kwanza, akashinda
katika baadhi ya mbio za barabarani barani Ulaya).
Alishinda medali ya fedha
katika Mbio za Mabingwa za Dunia za IAAF mwaka 2007, akimaliza wa pili nyuma ya
Lornah Kiplagat aliyevunja rekodi ya dunia. Ameolewa na Mkenya mwenzake mwanamichezo,
Charles Koech, mwishoni mwa mwaka 2007 na walipata mtoto, Jared Kipchumba 2008.
Baada ya mwaka kuwa nje, alirudi katika mashindano ya Dunia ya 10k Bangalore
Mei 2009. Alimaliza wa pili nyuma ya mshindi, Aselefech Mergia, lakini akaweka rekodi
mpya ya ubora ya 32:09 katika km 10. Septemba mwaka huo, alimaliza kwa 1:07:00 katika mashindano ya 2009 ya Nusu Marathoni ya Lille , ambayo ilikuwa ni alama ya ushindi na akawa wa
saba kwa kasi katika muda wote.
Mashindano ya Lille ilimaanisha kuwa alifuzu kwa Mashindano ya Dunia ya
Mabingwa ya Nusu Marathoni ya IAAF 2009 mjini Birmingham . Alimshinda Aberu Kebede katika ushindi wake wa
kwanza wa michuano ya Dunia, akaweka rekodi mpya ya ubora ya saa 1:06:36 na kuvunja rekodi ya michuano. Pia alichukua medali
ya dhahabu ya pili kama sehemu ya kikosi cha ushindi cha Kenya katika mashindano ya timu. Muda wake wa km 15 wa dakika
46:51, ni bora zaidi kuliko rekodi ya dunia iliyowekwa na Kayoko Fukushi wa
Japan ya 46:55. Muda wake ulikuwa wa pili kwa kasi kwa muda wote katika nusu
marathon (baada ya Lornah Kiplagat) na mkurugenzi wa New York City Marathon,
Maria Wittenberg, alitabiri kwamba Keitany anaweza kuwa bora ulimwenguni katika
marathon katika miaka ijayo. Nusu marathon ilikuwa rekodi mpya ya Afrika,
rekodi ya awali ya saa 1:06:44 , iliwekwa na Elana Meyer wa Afrika Kusini mwaka 1999. Pia aliishinda
rekodi ya bingwa aliyemtangulia wa Kenya ya saa 1:06:48 aliyoiweka huko Udine
miaka miwili kabla.
Alishinda mbio za 2010 za Nusu
Marathon za Abu
Dhabi . Pia
alishinda mbio za 2010 za Berlin
25K, akiweka rekodi mpya ya dunia kwa saa 01:19:53 . Rekodi ya awali ilikuwa inashikiliwa na Mizuki Noguchi wa Japan tangu
mwaka 2005. Alitumia mbio za Nusu Marathon za Ureno mwezi Septemba kama maandalizi kwa mbio za New York na kuongoza kuanzia mwanzo na kushinda kwa muda wa saa
1:08:46 . Katika ukimbiaji wake wa kwanza katika Marathon za 2010 NYC alikuwa miongoni mwa watu watatu walioongoza lakini alishindwa
katika hatua za mwisho kukamilisha katika saa 2:29:01 na kushika nafasi ya tatu.
Keitany aliuanza 2011 kwa
kuvunja rekodi aliposhinda Nusu Marathon za Ras Al
Khaimah na kuweka rekodi ya dunia ya 01:05:50 . Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa mwanamke kukimbia kwa chini ya dakika
66 na kuweka rekodi kadhaa zingine baadaye, ikiwa ni pamoja na rekodi ya dunia
ya 1:02:36 kwa km 20 na ile ya km 8 na maili 10. Kisha
alishinda katika marathoni za 2011 za London katika muda wa saa 02:19:17 , na kuwa wa nne kwa kasi katika muda wote kwa wanawake.
Alishinda kwa mara ya pili katika mbio za Nusu Marathoni za Ureno na kuboresha
rekodi yake mwenyewe kwa saa 1:07:54 .
Alikusudia kuboresha rekodi
yake ya dunia ya Nusu Marathoni ya 2012 RAK, lakini hali ya upepo ilimfanya
kutumia muda wa saa 1:06:49 akishinda kwa muda zaidi kuliko mwaka uliopita.
Makala haya yameandaliwa na Bishop Hiluka kwa msaada
wa vyanzo mbalimbali vya habari.
No comments:
Post a Comment