Macky Sall
ALIYEKUWA rais wa Senegal , Abdoulaye Wade, amekubali kushindwa na mpinzani
wake, Macky Sall, katika dura ya pili ya uchaguzi wa Urais huku hirika la habari
la serikali nchini Senegal likitoa habari za kukubali kwake kushindwa.
Wade alimpigia simu mpizani
wake Macky Sall, na kumuambia kuwa amekubali kushindwa. Na maelfu ya wafuasi wa
Macky Sall walijitokeza katika barabara za mji wa Dakar wakisherehekea ushindi wa kiongozi wao.
Miongoni mwa waliokuwa
wakisherehekea ni Bi Seynabou Seck ambaye alishindwa kuficha furaha yake kwa
kusema kuwa: "Niimefurahi sana , Macky bado ni kijana na tena ni mtu mpole sana na ana heshima! Kwa hakika anastahili ushindi huu.
Kila mtu alikuwa akimuombea ashinde”.
Mshindi huyo wa duru hiyo
ya pili ya uchaguzi wa urais ameutaja ushindi wake kama muamko mpya kwa raia wa Senegal . Macky Sall aliyazungumza hayo mara tu baada ya
mpinzani wake Abdoulaye Wade mwenye umri wa 85 kukubali kuwa ameshindwa katika
duru hiyo ya pili.
Wade alikuwa anataka
kuchaguliwa tena kama raia wa Senegal kwa muhula mwengine wa tatu baada ya kubadilisha
katiba ya nchi hiyo. Mabadiliko hayo yalizua machafuko na vurugu kubwa nchini
humo.
Machafuko hayo yalishtua
ulimwengu kwani tofauti na jirani zake Senegali imekuwa tulivu na haijawahi
kuwa na mapinduzi ya kijeshi kama jirani zake. Lakini upinzani ulipinga hatua ya
kiongozi wao mkongwe na kwenda mahakamani. Hata hivyo, mahakama iliidhinisha
hatua ya Wade ya kubadili katiba ili aweze kusimama tena kama rais.
Na baada ya duru ya kwanza
kukosa kuwa na mshindi wa moja kwa moja kwani hakuna aliyepata zaidi ya
asilimia 50, ikiwa ni lazima kuwe na duru ya pili ambapo viongozi wote wa
upinzani walimuunga mkoni Macky Sall.
Na sasa Macky Sall ambaye
zamani alikuwa Waziri mkuu katika serikali ya Abdoulaye Wade ameibuka mshindi.
Historia yake
Macky Sall amezaliwa 11
Desemba 1961. Anatarajiwa kuapishwa rasmi kuwa rais keshokutwa, Jumapili tarehe
1 Aprili 2012. Aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Senegal kuanzia Aprili 2004 hadi Juni 2007 na alikuwa Rais
wa Bunge la Senegal kuanzia Juni 2007 hadi Novemba 2008. Alikuwa Meya
wa Fatick kuanzia 2002 hadi 2008 na kushikilia tena nafasi hiyo tangu Aprili
2009.
Sall alikuwa mwanachama wa
muda mrefu wa chama kilichotawala cha Senegal Democratic Party (PDS). Baada ya
kuingia katika mgogoro na Rais Abdoulaye Wade, aliondolewa kutoka katika
wadhifa wake kama Rais wa Bunge mwezi Novemba 2008, hivyo alianzisha
chama chake mwenyewe na kujiunga na upinzani. Amejitokeza kuwa Rais wa Senegal tarehe 25 Machi 2012 baada ya kuishinda tawala
katika uchaguzi wa marudio.
Sall, mhandisi wa jiolojia
ki taaluma, alizaliwa katika eneo la Fatick. Alikuwa Katibu Mkuu wa PDS wa Mkoa
wa Fatick mwaka 1998 na aliwahi kuwa Katibu wa Taifa wa PDS mkuu wa Madini na
Viwanda. Alikuwa Mshauri Maalum wa Nishati na Madini kwa Rais Abdoulaye Wade kuanzia
Aprili 6, 2000 hadi Mei 12, 2001, pamoja na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Mafuta ya Senegal (PETROSEN) kuanzia Desemba 13, 2000 hadi Julai 5, 2001. Kisha
akawa Waziri wa Madini, Nishati na Hydraulics mnamo Mei 12, 2001, na
alipandishwa cheo na kuwa Waziri wa Nchi, lakini akiendelea na nafasi yake
nyingine, tarehe 6 Novemba, 2002. Pia alikuwa Meya wa Fatick Juni 1, 2002.
Mnamo Agosti 27, 2003, Sall
alihamishwa kutoka nafasi yake kama Waziri wa Nchi anayeshughulikia pia Madini, Nishati
na Hydraulics na kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Jumuiya za Mitaa, wakati pia akiwa
msemaji wa serikali. Kisha aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu na Rais Wade Aprili 21,
2004, wakati mtangulizi wake, Idrissa Seck, alipofukuzwa. Aprili 25, 2004, Seck
akawa Makamu wa Rais wa PDS wa kamati ya uendeshaji.
Sall aliwahi kuwa
mkurugenzi wa kampeni za Wade wakati wa uchaguzi katika uchaguzi wa rais wa Februari
mwaka 2007, ambao Wade alishinda, akipata wingi wa kura katika raundi ya kwanza
tu. Baada ya Wade kuapishwa, Sall aliwasilisha hati ya kujiuzulu kwake Aprili
10 na mara moja aliteuliwa tena.
Rais wa Bunge
Katika uchaguzi wa wabunge wa
Juni 2007, Sall alichaguliwa kwenye Bunge kama mgombea katika orodha ya taifa ya Muungano wa Sopi. Baada ya uchaguzi,
Wade alimteua kuwa Cheikh Hadjibou Soumaré kuwa Waziri Mkuu wa Juni 19, akichukua
nafasi ya Sall, ambaye alikuwa amejiuzulu pamoja na serikali yake muda mfupi
kabla. Sall alisema kuwa aliona fahari kwa kile alichokifanya wakati akiwa
Waziri Mkuu.
Sall alichaguliwa kuwa Rais
wa Bunge siku moja baadaye, mnamo Juni 20, 2007, alikuwa mgombea pekee na
alipata kura 143 kutoka kwa manaibu 146 ya sasa. Sall na Wade wakaingia katika
migogoro baadaye mwaka 2007 wakati Sall alipomuita mtoto wa Wade Karim, Rais wa
Wakala wa Taifa wa Shirika la Kiislam (OIC), kwa ajili ya kusikilizwa katika
Bunge kuhusu maeneo ya ujenzi jijini Dakar kwa Mkutano wa OIC uliopangwa kufanyika huko Machi
2008. Hii ilichukuliwa kama jaribio la Sall kutaka kudhoofisha nafasi ya Karim
na uwezekano wa kushawishi ili kujijengea nafsi yake ya kuwania urais,
kuchochea uadui wa Wade na wafuasi wake ndani ya PDS.
Mnamo Novemba 2007, Kamati ya
Uendeshaji ya PDS iliifutwa nafasi ya Sall ya Naibu Katibu Mkuu, ambayo ilikuwa
ya pili kwa madaraka katika chama, na hivyo kamati hiyo iliamua kuwasilisha muswada
katika Bunge ambao uliomba kupunguza muda wa Rais wa Bunge wa kutoka miaka
mitano hadi mwaka mmoja. Kufuatia kifo cha kiongozi wa kidini wa Mourides,
Serigne Saliou Mbacké, mwishoni mwa Desemba 2007, mrithi wake, Serigne
Mouhamadou Lamine Bara Mbacké, alimuomba Wade kumsamehe Sall; Wade baadaye
alikutana na Sall na wawili walisemekana kupatana mwanzoni mwa Januari 2008.
Sall alibaki katika
msuguano na uongozi wa PDS mwaka 2008.
Mwezi Septemba 2008, naibu wa PDS aliwasilisha muswada wa kupunguza muda
wa Rais wa Bunge kwa mwaka mmoja, na baadaye katika mwezi huo, Sall aliitwa
mbele ya Kamati ya Nidhamu ya PDS, ingawa hakujitokeza. Kwa jambo hili, Sall
alishitakiwa kwa mipango binafsi ya kuleta mgawanyiko ndani ya chama, pia alidaiwa
kufanya "kwa lengo la kudhoofisha chama na nchi", ikimaanishwa hasa
kwa ziara ya Sall kwa Seneti ya Ufaransa na Mkataba wa 2008 wa chama cha Democratic
nchini Marekani. Taarifa iliyotolewa na mshauri wa Sall wa kisiasa ililaani
hatua ya kumuadabisha Sall kama "jaribio la kutaka kumfilisi kisiasa".
Oktoba 13, 2008, Bunge
lilipiga kura ili kupunguza muda wa Rais wa Bunge kuwa mwaka mmoja, hii
ilithibitishwa na Rais Wade Oktoba 21. Pamoja na jitihada za Sall kulinda
nafasi yake, Bunge lilipiga kura ya kumfukuza katika nafasi hiyo ya Rais wa
Bunge Novemba 9, 2008. Kulikuwa na kura 111 zilizotaka aondolewe na 22 dhidi ya
kitendo hicho. Sall mara moja alitangaza kuwa anajiuzulu katika PDS; uamuzi huu
ulimaanisha kwamba alikuwa anapoteza kiti chake katika Bunge, pamoja na kiti
chake katika baraza la halmashauri ya manispaa ya Fatick na wadhifa wake kama Meya wa Fatick. Pia alisema kuwa angeunda chama kipya. Seck Mamadou
alichaguliwa kuchukua nafasi ya Sall kama Rais wa Bunge
la Novemba 16, 2008.
Katika upinzani
Sall ilianzisha chama chake
mwenyewe, Alliance for the Republic–Yaakaar, mwanzoni mwa Desemba
mwaka 2008. Wizara ya Mambo ya Ndani ilimtuhumiwa Sall kujihusisha na fedha haramu
Januari 26, 2009; Sall alikanusha na kusema kuwa mashtaka yalikuwa ya kisiasa.
Mwishoni mwa Februari 2009 iliamuliwa kutomshitaka Sall kutokana na kukosekana
kwa ushahidi.
Kufuatia uchaguzi wa Machi
2009 wa halmashauri ya Fatick, Sall alichaguliwa tena katika nafasi yake ya
mwanzo ya Meya mwezi Aprili 2009. Alipata
kura 44 kutoka kwa madiwani 45 wa manispaa wa wakati huo; madiwani watano wa
Muungano wa Sopi hawakuwepo kupiga kura
Kampeni ya urais wa Senegal 2012
Matokeo ya awali ya
uchaguzi wa rais Februari 26, 2012 yalionesha Sall kupata asilimia 26.5 ya kura
dhidi ya 34.8 za Wade, na kulazimisha kurudiwa.
Katiba na uchaguzi
Sall anapenda kurejea
kwenye mipaka ya awali ya muda wa urais. Katika mzunguko wa pili wa uchaguzi wa
rais, Sall alitoa wito kwa wagombea wengine wote walioshiondwa kumsaidia na kumuacha
Youssou N'Dour kwa sababu aliahidi kurejesha muda wa miaka mitano kutoka muhula
uliopita wa miaka saba ambao Wade alitaka urejeshwe, pia alisema atahakikisha
kwamba hakuna kiongozi anaweza kubaki madarakani kwa zaidi ya vipindi viwili.
Makala haya yameandaliwa na Bishop Hiluka kwa msaada
wa vyanzo mbalimbali vya habari vya kimataifa.
No comments:
Post a Comment