Joyce Banda
ALIYEKUWA makamu wa Rais wa
Malawi , Joyce Banda, amechukua madaraka ya kuiongoza nchi
hiyo ya Kusini mwa Afrika Jumamosi ya Aprili 6, mwaka huu kufuatia kifo cha Rais Bingu wa Mutharika. Banda ambaye hana undugu na Rais wa kwanza wan
chi hiyo, Hayati Dk. Kamuzu Banda anakuwa rais wa kwanza mwanamke Kusini mwa Jangwa la Sahara, na
aliapishwa mbele ya bunge katika mji mkuu wa Malawi, Lilongwe.
Banda, ambaye alikuwa makamu wa rais tangu mwaka 2009, alishangiliwa na
kupigiwa makofi kabla na baada ya shughuli hiyo. Mutharika, 78, alipatwa na mshtuko wa moyo siku ya Alhamisi, ingawa
kifo chake hakikuthibitishwa hadi Jumamosi.
Kuchelewa kutangazwa kifo
chake kulisababisha wasiwasi kuhusu nani anaongoza nchi hiyo. Kulikuwa na
tetesi kuwa watu wa karibu wa Rais Mutharika walikuwa wakitaka kubadili katiba
ya nchi ili kumzuia Banda kuchukua madaraka, na badala yake kumpa ndugu wa rais,
Peter Mutharika ambaye ni waziri wa mambo ya nje wadhifa huo.
Katiba ya Malawi inataja kwamba makamu wa rais atachukuwa madaraka ya
nchi iwapo rais amefariki dunia lakini ilionekana kwamba Mutharika alikuwa
akimuandaa mdogo wake Peter kuwa mrithi wake.
Banda alifarakana na Rais
Mutharika mwaka 2010 na kisha kuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wake. Alifukuzwa
kutoka chama cha DPP na kuunda chama chake cha Peoples Party.
Hofu ya kuzuka kwa
mapambano ya kuwania nafasi ya kumrithi rais huyo imeanza kupungua kutokana na
asasi za kitaifa kuunga mkono makabidhiano ya madaraka kwa kuzingatia katiba.
Serikali imethibitisha rasmi kifo cha Mutharika mwenye umri wa miaka 78 hapo
Jumamosi ikiwa ni siku mbili baada ya kufariki kwake dunia kutokana na mshtuko
wa moyo.
Banda mwenye umri wa miaka
61 alikuwa na mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Lilongwe ambapo alitangaza siku 10 za maombolezo rasmi ya
Mutharika ambaye aliitawala Malawi kwa miaka minane. Ameamuru bendera za taifa kupepea
nusu mlingoti na shirika la utangazaji la taifa kupiga muziki wa kuhuzunisha.
Ametowa wito kwa Wamalawi
kuwa watulivu na kudumisha amani katika kipindi hiki cha maombolezo. Banda
alikuwa akizungumza huku akiwa ameandamana na mwanasheria mkuu wa serikali na
wakuu wa jeshi na polisi.
Kabla ya kuchukua rasmi
madaraka hayo aliulizwa na mwandishi wa habari iwapo alikuwa anachukuwa
madaraka ya urais, Banda mwanaharakati wa haki za wanawake alijibu "kama unavyoona, katiba inafaya kazi".
Banda anatazamiwa kuiongoza
nchi hiyo hadi uchaguzi ambao umepangwa kufanyika hapo mwaka 2014. Ofisi ya rais
na baraza la mawaziri vimetoa taarifa yenye kuwahakikishia raia na jumuiya ya
kimataifa kwamba katiba ya Jamhuri ya Malawi itaheshimiwa ipasvyo katika kuongoza kipindi cha
mpito.
Historia yake
Joyce Hilda
Banda ni mwelimishaji na mwanaharakati wa haki za jinsia kwa watu wa
chini. Alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi kuanzia mwaka 2006 hadi 2009 na Makamu wa Rais wa Malawi kuanzia Mei 2009 kabla
ya kuukwaa urais Aprili 7, 2012.
Pia alikuwa Mbunge na
Waziri wa Jinsia, Mambo ya Watoto na Huduma za Jamii. Kabla ya kushiriki kikamilifu
katika siasa alikuwa mwanzilishi wa Taasisi ya Joyce Banda (Joyce Banda
Foundation), mwanzilishi wa Chama cha Taifa cha Wafanyabiashara Wanawake
(NABW), Mtandao wa Viongozi Vijana Wanawake na Mradi Njaa. Alitajwa katika
jarida la Forbes mwaka 2011 kama mwanamke wa tatu mwenye nguvu zaidi na ushawishi
katika Afrika.
Ni mwanzilishi na kiongozi
wa Chama cha Watu (People's Party) kilichoundwa
mwaka 2011, na kabla ya kifo cha Bingu wa Mutharika alionekana kuwa na uwezekano
wa kugombea Urais wa Malawi katika uchaguzi mkuu wa 2014. People's
Party wamepanga kuwa na mkataba baadaye mwaka huu, pamoja na uwezekano wa
kuthibitishwa kwa Joyce Banda kuwa kiongozi wa chama.
Maisha ya awali
Banda anatokea Malemia, kijiji katika Wilaya ya Zomba nchini Malawi. Ana cheti cha
Cambridge . Ana Shahada ya Sanaa katika Elimu ya Mafunzo
kutoka Chuo Kikuu cha Columbus ,
na Diploma katika Usimamizi aliyopata nchini Italia. Katika umri wa miaka 25,
alikuwa na watoto watatu na alikuwa akiishi mjini Nairobi , Kenya . Mwaka 1975, harakati za wanawake nchini Kenya zilimtia moyo Banda na aliwachukua watoto wake na
kuachana na ndoa yake ya kwanza ya unyanyasaji. Kati ya 1985 na 1997 Banda
alianzisha biashara na makampuni mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ndekani Garments,
(1985), Akajuwe Enterprises (1992), na Kalingidza Bakery (1995). Mafanikio
yake yalimuongoza kuwasaidia wanawake wengine kufikia uhuru wa kifedha na
kuvunja mizunguko ya kunyanyasika na umaskini.
Ni dada wa Anjimile Oponyo, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Raising
Malawi Academy for Girls iliyoanzishwa na Madonna. Ameolewa na Richard Banda, aliyekuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Malawi .
Maisha ya Siasa (2004-2009)
Kabla ya kuwa mwanamke wa
kwanza kuwa Makamu wa Rais na baadaye Rais, alikuwa Mbunge wa jimbo la Zomba-Malosa. Pia
alikuwa Waziri wa Huduma za Jinsia, Ustawi wa Watoto na Jumuiya kabla ya
kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Rais Bingu wa Mutharika Juni 1, 2006. Kama
Waziri wa Jinsia, Ustawi wa Watoto na Huduma za Jamii alipigania hadi kutungwa Sheria
ya Unyanyasaji wa kijinsia, ambayo ilishindwa kwa miaka saba kabla. Aliunda
Jukwaa la Taifa la Usaidiaji wa Yatima na walio kwenye mazingira magumu na
Kampeni ya Kutovumilia dhidi ya unyanyasaji wa watoto.
Makamu wa Rais (2009-2012)
Banda alikuwa mgombea
mwenza wa urais wa chama cha Democratic Progressive (DPP)
katika uchaguzi wa Rais Mei 2009, akigombea
sambamba na Mutharika, mgombea urais wa DPP. Kwa mshangao ndani ya DPP,
Joyce Banda na makamu wa pili wa rais, Khumbo Kachali, walifukuzwa kama makamu wa Rais wa DPP tarehe 12 Desemba 2010 kwa kile kilichojulikana
'kupambana na chama hicho’. Katika majaribio ya kumdhoofisha, rais aliendelea
kutoa majukumu ambayo awali yalikuwa chini ya Banda na kuyakabidhi kwa Callista Mutharika ambaye aliingizwa katika
baraza la mawaziri mwezi Septemba 2011.
Uhusiano kati yake na Rais wa Malawi uliendelea kuwa wa wasiwasi kwa
sababu ya Rais kujaribu kumpa nafasi ndugu yake, Peter Mutharika kama mwandamizi wa chama na
rais mtarajiwa. Ingawa Banda alitimuliwa kutoka nafasi ya Makamu wa Rais
wa DPP pamoja na Makamu wa
Rais wa pili Khumbo Kachali, aliendelea kuwa Makamu wa Rais wa Malawi kama
ilivyoainishwa katika katiba ya Jamhuri ya Malawi. Hatua hii ilisababisha
wengi kujitoa DPP na kuunda mitandao ambayo ilimsaidia makamu wa rais ili
kusaidia ugombea wake wa ur ais wa Malawi katika uchaguzi mkuu wa 2014. DPP
ilikanusha kujitoa kwa wengi na kusisitiza kwamba waliojitoa walikuwa wachache
tu.
Urais
Baada ya kifo cha Mutharika,
kulikuwa na hofu ya kugombea madaraka kufuatia taarifa ya Waziri wa Habari na
Elimu ya Uraia, Patricia Kaliati, kuwa "mwenendo wa Joyce
Banda ni katika kutengeneza chama chake cha upinzani kimsaidie katika
kufanikiwa urais." Shirika la habari la Ufaransa lilitoa taarifa kuwa
rais wa zamani wa Malawi, Bakili Muluzi, kusisitiza “utaratibu wa kufuata
katiba,” akisema makamu wa rais lazima achukue madaraka moja kwa moja kwa
mujibu wa katiba. “Natoa wito kufuata kikatiba, kwa ajili ya amani
kuendelea na utaratibu. Sheria za Malawi ziko wazi kabisa kuwa makamu wa rais anachukua madaraka”
pale ambapo hayupo rais. Tunatakiwa kuzuia hali ambapo kuna
machafuko. Hebu tufuate katiba. Hatuna chaguo zaidi ya kufuata
katiba. Ni muhimu sana
kuwepo amani na utulivu,” alisema.
Vikosi vya Usalama vya Malawi pia vilitaka katiba ifuatwe.
Chama cha wanasheria wa
Malawi pia kilithibitisha kuwa chini ya kifungu cha 83 (4) cha katiba ya Malawi, Banda ndiye
mrithi halali wa Urais. Aliapishwa kama rais mwanamke wa kwanza nchini humo
Aprili 7, na kutoa wito kwa umoja wa kitaifa. Alipongezwa na Rais wa Zimbabwe , Robert Mugabe .
Makala haya yameandaliwa na Bishop Hiluka kwa msaada
wa vyanzo mbalimbali vya habari vya kimataifa.
No comments:
Post a Comment