Jun 1, 2012

C. ODUMEGWU OJUKWU: Aliyetaka Biafra ijitenge nchini Nigeria azikwa

Kanali Chukwuemeka Odumegwu-Ojukwu

NNEWI
Nigeria

MAELFU ya watu kusini mashariki mwa Nigeria wamehudhuria mazishi ya kiongozi wa zamani wa vuguvugu la Biafra, Kanali Chukwuemeka Odumegwu-Ojukwu. Nyumbani kwa Ojukwu mjini Nnewi, watu wenye mapenzi mema walipanga mistari mitaani na kupanda majengo marefu ili waweze kuona.

Kanali Ojukwu alikufa nchini Uingereza mwaka jana baada ya kuugua kwa muda mrefu akiwa na miaka 78. Kujitangazia kwake uhuru wa Biafra mwaka 1967 kulizusha vita vya wenyewe kwa wenyewe na watu zaidi ya milioni moja walikufa.

Ojukwu anabakia kuwa nguzo mtu maarufu katika siasa za Nigeria, akiwania Urais wa nchi hiyo mara mbili katika miaka ya 2000.

Historia yake

Chukwuemeka Odumegwu Ojukwu alizaliwa 4 Novemba 1933, alikuwa afisa na mwanasiasa wa Nigeria. Ojukwu aliwahi kuwa mkuu wa kijeshi wa Kanda ya Mashariki mwa Nigeria mwaka 1966, kiongozi aliyeongoza mgawanyiko wa kutaka Jamhuri ya Biafra mwaka 1967 hadi 1970 na mwanasiasa wa Nigeria kuanzia 1983 hadi 2011, alipokufa, akiwa na umri wa miaka 78.

Kazi

Ojukwu alifikia umaarufu wa kitaifa baada ya uteuzi wake kama mkuu wa kijeshi mwaka 1966, na kazi zake baada ya hapo. Mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali ya kiraia ya shirikisho la Nigeria mnamo Januari 1966 na mapinduzi ya Julai 1966 ya makundi mbalimbali ya kijeshi, yaliyodhaniwa kuwa mapinduzi ya kikabila, yaliyosababisha uuaji wa kikatili wa jumuiya ya watu wa Igbo Kaskazini mwa Nigeria ambapo wengi wao waliuawa. Ojukwu ambaye hakushiriki moja kwa moja katika mapinduzi aliteuliwa mkuu wa kijeshi wa Kanda ya Mashariki nchini humo mwezi Januari 1966 na Jenerali Aguyi Ironsi.

Mwaka 1967, changamoto kubwa iliwakabili kabila la Igbo wa Nigeria kwa mapinduzi ya kijeshi ya Januari 15, 1966 yakiongozwa na Chukwuma Kaduna Nzeogwu aliyechukuliwa sana kuwa mwelewa mzuri na akazikwa kwa heshima kamili ya kijeshi alipouawa na wale aliopigana nao.

Mapinduzi yake ya kijeshi yalisababisha uasi wa kisiasa na uporaji katika mitaa ya Magharibi mwa Nigeria.  Kwa bahati mbaya Sarduana wa Sokoto, Ahmadu Bello: Waziri Mkuu wa Nigeria, Tafawa Balewa: Mkuu wa Mkoa wa Magharibi, Chifu Akintola Ladoke na Waziri wa Fedha, Chifu Festo Okotie Eboh (kati ya watu wengine ikiwa ni pamoja na maofisa wa kijeshi) waliuawa katika mchakato. mauaji ya kikatili wa jumuiya ya watu wa Igbo yalifuatia katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria mwanzoni mwaka Julai 1966. Hatimaye, aliyekuwa Luteni Kanali Odumegwu Ojukwu alitangaza Uhuru wa Biafra tarehe 30 Mai 1967.

Alishiriki katika mazungumzo ya kutafuta kumaliza uhasama kwa kutafuta amani na uliokuwa uongozi wa kijeshi wa Nigeria, ulioongozwa na Jenerali Yakubu Gowon (kiongozi wa kijeshi nchini Nigeria kufuatia mapinduzi ya Julai 1966). Viongozi wa kijeshi walikutana Aburi Ghana (Mkataba wa Aburi), lakini makubaliano yaliyofikiwa hapo hayakutekelezwa kwa pande zote kuridhia waliporudi Nigeria.

Kushindwa kufikia makubaliano ya kufaa, uamuzi wa uongozi wa kijeshi wa Nigeria ulianzisha majimbo mapya katika Kanda ya Mashariki na mauaji ya kikatili yakaendelea Kaskazini mwa Nigeria yaliyomuongoza Ojukwu kutangaza kujitenga kwa Kanda ya Mashariki chini ya jina jipya la Jamhuri ya Biafra mwaka 1967. Matukio haya yakasababisha vita vya kiraia nchini Nigeria. Ojukwu aliongoza vikosi vya Biafra, na kushindwa kwa Biafra Januari 1970, na baada ya kutoa maelekezo kwa Philip Effiong alikwenda uhamishoni kwa miaka 13, akarejea Nigeria kufuatia msamaha.

Maisha ya awali na elimu

Chukwuemeka "Emeka" Odumegwu-Ojukwu alizaliwa tarehe 4 Novemba 1933 katika eneo la Zungeru Kaskazini mwa Nigeria katika familia ya Louis Odumegwu Ojukwu , mfanyabiashara kutoka Nnewi, Jimbo la Anambra Kusini-Mashariki mwa Nigeria. Louis alikuwa katika safari za biashara; alichukua nafasi ya kupata faida kwa kuongezeka kwa biashara wakati wa Vita ya Pili ya Dunia na kuwa mmoja wa watu tajiri nchini Nigeria. Alianzia elimu yake Lagos, Kusini Magharibi mwa Nigeria.

Mwaka 1944, alifungw jela kwa kumshambulia mwalimu mzungu wa koloni la Uingereza ambaye alimfedhehesha mwanamke mweusi katika Chuo cha Mfalme mjini Lagos, tukio ambalo lilienea katika magazeti.  Katika umri wa miaka 13, baba yake akampeleka nje, nchini Uingereza kusoma, kwanza katika Chuo cha Epsom na baadaye Chuo cha Lincoln, Chuo Kikuu cha Oxford, ambapo alipata shahada ya uzamili katika historia. Alirejea katika koloni nchini Nigeria mwaka 1956.

Kazi ya mwanzo

Alijiunga na utumishi wa umma Mashariki mwa Nigeria kama Afisa Tawala wa Udi, ambayo kwa sasa inajulikana kama Jimbo la Enugu. Mwaka 1957, katika miezi ya kufanya kazi katika serikali ya ukoloni, aliondoka na kujiunga na jeshi kama mmoja wa wahitimu wa kwanza wachache wa chuo kikuu kujiunga na jeshi: O. Olutoye (1956); C. Odumegwu Ojukwu-(1957), EA Ifeajuna na CO Rotimi (1960), na A. Ademoyega (1962).

Historia ya Ojukwu na elimu vilimhakikishia kupanda hadi safu ya juu. Wakati huo, Jeshi la Nigeria lilikuwa na maafisa 250 na 15 tu ndiyo walikuwa Wanigeria. Kulikuwa na safu nyingine 6,400, ambapo 336 walikuwa Waingereza.  Baada ya kutumikia katika jeshi la  Umoja wa Mataifa la 'kulinda amani nchini Congo, chini ya Meja Jenerali Johnson Thomas Aguiyi-Ironsi, Ojukwu alipandishwa cheo na kuwa Luteni Kanali mwaka 1964 na kupelekwa Kano, ambapo alikuwa kiongozi wa Kikosi cha 5 cha Jeshi la Nigeria.

Kifo

Tarehe 26 Novemba 2011, Ikemba Odumegwu Ojukwu alifariki nchini Uingereza baada ya kuugua kwa muda mrefu, alikuwa na umri wa miaka 78. Jeshi la Nigeria lilimpa heshima ya juu ya kijeshi na kufanya gwaride la mazishi kwa ajili yake mjini Abuja, Nigeria tarehe 27 Februari siku mwili wake uliporudishwa Nigeria kutoka London kabla ya mazishi yake siku ya Ijumaa, Machi 2, 2012.

Alizikwa katika kiwanja chake katika eneo la Nnewi. Kabla ya safari yake ya mwisho, ilikuwa ni maombolezo ya kipekee zaidi na yaliyochukua wiki nzima ya mazishi nchini Nigeria kando ya Chifu Obafemi Awolowo, ambapo mwili wake ulibebwa karibu majimbo mengi hasa majimbo matano ya Mashariki, IMO, Abia, Enugu, Ebonyin, Anambra, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wan chi hiyo, Abuja na Jimbo la Niger alikozaliwa.

Makala haya yameandaliwa na Bishop Hiluka kwa msaada wa vyanzo mbalimbali vya habari vya kimataifa.

No comments:

Post a Comment